MSICHANA ANAYEDAI KUBAKWA NA MBUNGE WA TANZANIA
 |
Flora Bahati Lyimo a.k.a Mbuta Nanga |
 |
Mbuta nanga |
Binti mrembo aitwaye Flora Bahati Lyimo anamtuhumu mbunge mmoja wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Akiendelea
kuweka wazi kisa hicho, Flora anasema: “Nikiwa kwenye mkutano….(jina la
mbunge) alinifuata akaniuliza nimeandika watu wangapi waliohudhuria
mkutano huo, nikamjibu 50 akaniambia niongeze idadi hiyo ili ionekane
mkutano ulikuwa na watu (Watanzania waishio Uingereza) wengi.
“Mkutano ulimalizika, sasa nilipokuwa naondoka kurudi nyumbani kwangu, mbunge huyo na wenzake nao walitoka.
Tukiwa njiani wenzake walikwenda kujisaidia haja ndogo, yeye akaniomba akajisaide nyumbani kwangu, nilimkubalia.
Alipofika
ndani, bila kujua kila kitu kinaonekana kwenye kamera alinibadilikia
kama vile adui vitani, ona sasa wema wangu ukawa umeniponza.
Alinirukia,
akaniburuza hadi kitandani kwangu. Nilipokuwa mkali na kwa namna
nilivyokuwa nimechanganyikiwa sishikiki ndipo akanivamia maungoni,
akanichania nguo zangu akitaka nimwachie atimize lengo lake la
kuniingilia kimwili kwa nguvu.
“Nilijitahidi ili
asifanikiwe, nikamwambia amekwisha kwani lazima nimwanike ndipo
akanipiga nusu aniue akisisitiza kuwa kama nitauanika uovu wake huo au
kuchukua hatua zozote ataniua.
“Inaniuma sana, kunibaka anibake halafu atishie kuniua, unyama gani huu?”
Flora anaendelea kusema:
“Katika
purukushani hiyo, nilipopata mwanya kidogo tu, nikapiga namba ya polisi
999 kuomba msaada. Alipoona hivyo alitoka na kutokomea kusikojulikana.
Polisi walipofika hawakufanikiwa kumkamata.”
Flora
alisema polisi walimchukua na kila kitu cha ushahidi zikiwemo nguo zake
hadi kituoni, wakamhoji kwa kumrekodi sauti, wakampa namba ya jalada la
kesi inayosomeka; 4621279/2012-UBAKAJI/KUTISHIA KUUA ambapo hadi leo
mbunge huyo anasakwa na Polisi wa London, akikanyaga tu Uingereza lazima
akamatwe akajibu tuhuma za ubakaji na kutishia kuua.
Flora akaongeza:
“Ukweli ni kwamba hakufanikiwa kukamatwa kwa sababu alikuwa na passport
za kidiplomasia ambazo nyingine hakutumia jina lake halisi.
“Januari mwaka huu
nilipotaka kurudi nyumbani Kilimanjaro, mahakama ya hapa (Uingereza)
ilinipa barua ambayo nilipofika niliipeleka Kituo Kikuu cha Polisi Moshi
nikafunguliwa faili Namba Mos/RB/17127/12 kwa ajili ya ulinzi chini ya
R.C.O Ramadhan Ng’anza.
“Niliwaeleza kuwa mtu anayetaka kuniua ni mbunge huyo. Kweli waliahidi
kunisaidia,
nilipoondoka kurudi London niliwasiliana na polisi Kilimanjaro lakini
niliona kama kuna kitu au mbunge huyo yupo juu ya sheria kwani walikana
kunifahamu.
“Sitachoka kutafuta haki na kutetea wanawake wanaobakwa kila siku wanaona
aibu kusema, naamini aibu haipo kwa mbakwaji bali kwa mbakaji, yule ….
Flora allisema kama kweli mbunge huyo ni mwanaume aende tena jijini London
kama hatasimamishwa kizimbani na kuozea jela.